HABARIKA NASI KIPITIA

twitterHALI tete katika jijini la Arusha muda huu,Polisi wanapiga mabomu ovyo,watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Soweto wakisubiri kuaga miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la kigaidi wametawanywa kwa mabomu.
Mbali na watu kutawanywa kwa mabomu hayo,Mbunge wa Arusha Mjini Godless Lema amenusurika kufa huku gari lake likiharibiwa vibaya na mabomu ya Polisi .Majeruhi kibao wakikimbizwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
Barabara kuu ya kuingia mjini imefungwa, mabomu yanapigwa kila kona jijini Arusha risasi za moto zinatumika.
Akizungumza katika eneo la tukio mmoja wa wahanga wa tukio hilo, Agnes Mosha anasema kwamba hajui walipo ndugu zake wawili waliokuwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuaga miili ya rafiki zao.
"Dada nisaidie nivuke barabara nikimbie Mount Meru nasikia kuna dada yangu amepigwa bomu na hali yake ni mbaya sana,siwezi kuvuka dada sina nguvu tena jamani"alilalamika Agnes na kisha akapoteza fahamu na kuanguka chini.
Hata hivyo baada ya Agnes kuanguka chini hakuweza kuinuka huku watu wakikimbia na kumkanyaga,kulingana na hali kuwa mbaya eneo hilo.
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI